Motivation

Tabia 20 Zinazomfanya Mwanaume Kuwa Dhaifu

Tabia 20 Zinazomfanya Mwanaume Kuwa Dhaifu

Tabia 20 Zinazomfanya Mwanaume Kuwa Dhaifu

Leo tunaenda kusoma takribani tabia 20 zinazoweza kumfanya mwanaume kuwa dhaifu na kushindwa kabisa kupafomu vizuri kwenye maisha yake ya kila siku.

Mambo ni mengi ila leo tutaangazia kwenye hizi chache, ishirini tu ambazo inaonekana inakuwa ngumu kwa kizazi hiki cha sasa kutokutana nayo kila iitwapo leo.

Uzuri ni kwamba, yote yanaepukika inahitajika utayari tu ilikuona matokeo chanya kwenye maisha. Labda, ni wewe, au unadhani rafiki au ndugu anafaa kuona hii makala, usisite kushea nae ili aone naye.

Haya sasa twende tutakaone nini nilichowandalia leo. No hard feelings, read and pass it on. Love.

Tabia 20 Zinazomfanya Mwanaume Kuwa Dhaifu

1. Kuangalia picha za utupu

Unapata faida gani kuangalia watu wakifanya mapenzi? Yani unatumia bando lako na muda wako kuangalia sehemu za siri za watu wengine? Ama utapata hasara gani kutokufanya hivo?

Kuangalia pono sio jambo jema na huharibu kabisa afya ya ubongo na jinsia. Matokeo yake ni ubongo kuzorota katika umbo, ukubwa, na uwiano wa kemika. Vile vile hupelekea kupungua kwa utenda kazi na nguvu za kiume. Tumia muda na bando lako katika kuangalia fursa zinazokuzunguka.

2. Kupiga punyeto

Unafanyaje tendo na akili yako? That’s too dangerous. Unaharibu uwezo wa kufukilia na utendaji kazi wa nyeti zako, brother. Usiogope wanawake.

3. Betting

Jifunze kula kwa jasho. Jiulize, kwa nini makampuni ya betting siku hizi ni mengi kulinganishwa na awali? Utaelewa ni kwa sababu kizazi hiki kimekuwa dhaifu.

Kizazi cha wazee wetu vitu hivi havikuwepo na hata kama vingekuwepo nadhani muitikio ungekuwa mdogo sana sababu walikuwa ni watu wa kazi, watu wa kuvuja jasho muda wote.

Hawakutegemea kulishwa na pesa za bahati nasibu. Jifunze kutoka kwao na utagundua ya kuwa umepoteza muda mwingi sana ambao ungekuwa na una panga mikakati itakayo kusaidia baadae. Muda bado upo, anza sasa.

4. Kula hovyo hovyo

Milo mitatu ndio milo ijulikanayo. Inashangaza sana mtoto wa kiume kuonekana anakula kula kila mara. Nini hutokea baadae? Before too much is enough. Acha sasa.

5. Kunywa hovyo hovyo

Drink when it’s necessary sio kama bata.

6. Kulalamika 

Ukilalamika, umekubali kuwa mhanga. Watachoka kukusikiliza na mwishowe utadharauliwa na mbaya zaidi utaonekana mzigo. Wewe ni kijana, jitume pindi nguvu bado zimo.

7. Kuishi kama ndege

Huna malengo, huna dira, hujui unataka nini kwenye maisha. Inafahamika mwanaume ndio kiongozi wa familia, ukikosa malengo leo inamaanisha huna kesho nzuri.

Kiongozi mzuri ni anaejua wapi anaelekea, jikusanye na weka malengo au lengo lako moja na lifuate mpaka kieleweke. Hakuna kinachoshindikana.

8. Hujiamini na kuwa na msimamo

Sikia, usipokuwa na msimamo hakuna atakayekuheshimu. Hata mwanamke wako anasubiri kuona ukiwa challenged, unasimamiaje kweli yako. Principals are what makes a man.

9. Huwezi kusema hapana

Upo tu, yaani kila kitu ukiombwa huwezi kataa. Sikia, have some standards. Sikufunzi uchoyo, ila unatoa hadi kitu chako cha mwisho ambacho kingeweza kukusaidia?

Au unpata nini ukitoa halafu unabaki unanung’unika nyuma ya migongo yao? Jifunze kusema hapana kwa kutumia lugha nzuri.

Read Next: Reasons Why Having Dreams and Goals is Important in Life

10. Kushindwa kuweka eye-contact

Yaani mwanaume unakaziwa jicho na mwanamke unakuwa wa kwanza kuangalia pembeni. Acha bhana. You invented her. Hii kitalaam ni kama bado unaishi kwenu, hununui chochote, hulipii bili yoyote, halafu mshua akuogope wewe.

Kutakuwa kuna udhaifu flani hivi nyeti sana. Lol. Be a confident man.

11. Kukosa maarifa

Huna cha kujivunia! Hata ule msemo wa ‘hata saa mbovu husema kweli’, wewe haukuhusu. Brother, invest in yourself. Bobea kitu. Iwe makenika, kupiga picha, kuchora. Kuwa na kitu dunia inajua uko vyema. Huko utapata thamani yako.

12. Kufanya mambo madogo kuwa makubwa

Kadri umri unvyoenda unagundua kuwa kubishana na kuoneshana umwamba ni upotevu wa muda. Usikasirike kizembe. Kontro emosheni zako.

13. Unakuwa na hisia za kiboya

Jifunze kuamua kwa kutumia logic. Kiumbe mwenye hisia ni rahisi kuchezewa na kuingizwa mkenge. Mfano mzuri, angalia wachezaji wenye hisia, huitwa watukutuku baadae na hulimwa kadi au kutolewa kabisa mchezoni. Jifunze kutoka kwao.

14. Kudharau wengine

Epuka hii dhambi. Heshimu kila mmoja. Bosi mpaka mtu wa chini. Ukikutana na watu, onyesha upendo. Heshima itakuheshimisha. Zingatia sana neno hilo la mwisho brother.

15. Kutozingatia afya

Utapungukiwa nguvu za kiume. Utaugua magonjwa lishe. Utamea kitambi kizembe. Sababu tu, unakula vibaya na hufanyi mazoezi n.k.

16. Kutokufanya mazoezi

Unakuwa dhaifu. Yaani unakuwaje na mkono laini kama wa mwanamke wako. Huwezi kusimama kwa muda mrefu. Huwezi kuhimili hari ngumu. Ukikimbizwa kidogo unapumlia juu. Jenga mwili wako, piga tizi – jiimalishe. Ikiwa ulemavu sawa, sio uzembe.

17. Kukosa nidhamu ya kimaisha

Yaani upo tu. Huwezi kujituma na kufanikisha jambo. Nikisema kujituma ni namaanisha kuamua jambo na kulifanya kikamilifu A-Z. Sio unaamua kujifunza ujuzi mpya na unakata tamaa siku ya 3.

18. Kukosa kujiamini

Hakuna mtu anapenda kufanya kazi na wasojiamini. Hakuna mwanamke anapenda njemba haijiamini. Work on your confidence. Ukiingia sehemu kuwa wewe na jiamini yule umejitengeneza.

19. Kushindwa kutumia vyema akili yako

Kuituma kuwaza kile unataka ili kutumia muda mwingi kukitekeleza. Kuwa na mawazo hasi muda wote na kushindwa kufanya jambo lolote la maana.

20. Kuwa na marafiki mzigo

Rafiki hakusaidii kitu, akiwa nacho anakubania. Ukiwa na shida hakusaidii. Kwenda club anakuita chap, kwenye fursa utamsikia yeye. Chagua marafiki unaotamani kuwa kama wao.

Ambao watakuambukiza roho ya upambanaji na kujisimamia. Tunaishi mara moja, ila hiyo mara moja inatosha sana kama tutaifanyia vyema.

Hitimisho

Mwanaume kamili ni kama simba, hateteleshwi hovyo. Ukiona kama umegushwa na tabia mojawapo iliyotajwa hapo juu, ni muda sasa wa kufanya mabadiliko.

Hujasoma makala hii kwa bahati mbaya, muda bado unawo. Anza sasa. Kuwa mwanaume alietimilika. Jitafute!

About the author

Kelvin Chaisson

My name is Kelvin Chaisson and I live around this little internet corner. I am a Journalist who loves blogging. Yes, I am not a bot, you can follow me on my social networks and be friends!

Leave a Comment